P0135
OXYGEN SENSOR HEATER CIRCUIT MALFUNCTION
Kiujumla code hii inaelezea kuwa Oxygen sensor ina tatizo
YALIYOMO- Oxygen sensor ni nini?
- Historia ya Oxygen sensor
- Kazi ya Oxygen sensor
- Kazi ya heater
- Ni nini cha kufanya kutatua tatizo hili
Ni sensor inayotumika kwenye aina nyingi za engine za gari na hufungwa sehemu ya exhale/exhaust ina waya nne(4) na chache zikiwa na waya mbili(2)
Kuna jamaa mmoja wa kuitwa Robert Bosch alikuwa ametulia zake maghetoni akawaza engine itawezaje kupata kitu ambacho kitakuwa kinaelekeza kiwamgo gani cha hewa kitachokuwa kinahitajika kuweza kulipua mafuta ndani ya chemba za piston ndio mwamba akaja na idea ya oxygen sensor hiyo ilikuwa miaka ya 1970's
Jomba akaunda oxygen sensor yake yenye waya mmoja na kumbuka kipindi hicho Oxygen sensor yake hiyo ilikuwa haitumii ECM
1980's ,utundu ukaongezeka wakaunda Oxygen sensor ya waya tatu(3)
Baadaye kidogo wataalamu wakaona mbona kama Oxygen sensor zinakufa wakatuliza akili wakagundua zinakufa kwa sababu ya joto linalopatikana pale kwenye exhaust na suluhisho ikawa ni kuongeza jambo ndani ya sensor,na ndio wakaweka heater sensor ndani ya oxygen sensor na pia wakaongeza idadi za waya kwenye sensor
NB:Ndani ya oxygen sensor kuna heater sensor
Kuisaidia oxygen sensor kufikia kiwango cha joto kinahohitajika kwa wakati na haraka kulingana na joto la exhaust ili kuweza kufanya kazi kwa ufasaha
- Kagua waya kuanzia kwenye ECM kuelekea kwenye oxygen sensor kama zinafika kikamilifu
- Pima Oxygen sensor kwa kutumia kifaa cha multimeter kwa kuweka waya mbili za multimeter kwenye waya za oxygen sensor upande wa chanya (+) na hasi (-) kama Oxygen sensor ni nzima inatakiwa itoe majibu ya 200LV(0.20V) kwenye multimeter(majibu yakiwa tofauti na hivyo badilisha sensor hiyo)
Comments
Post a Comment