Valvematic

Valvematic
VALVEMATIC


Injini nyingi zinazotumia mafuta ya petrol hutumia throttle kawaida kuruhusu na kuzuia hewa inayoingia kwenye chemba za piston ila hapa sasa kuna utofauti kidogo kwenye injini inayotumia mfumo wa Valvematic hapa hewa inasimamiwa na valve(inlate valve)
Na hata hivyo sio kwamba throttle inatolewa kabisa kwenye mfumo hapana ila inatumika mara chache sana katika kufungua na kufunga .Mbadala wa throttle unakuwa ni valve za kuingiza (inlet valve) zenyewe sasa ndio zinafanya kazi ya kufungua na kufunga,hii inasababisha injini kuwa na ufanisi mzuri sana kwenye ulaji wa mafuta
Pata picha Injini ya 2.0 Valvematic inaboresha ulaji wa mafuta kwa 5-10%,huongeza utendani kwa 10% na inapunguza uzalishaji wa C02 (Carbon dioxide)
Toyota Corolla ya 2014 ni gari la kwanza kuuzwa Amerika Kaskazini kuwa na vifaa vya teknolojia ya Valvematic.

Comments

Popular posts from this blog

P1603 Engine stall history