Code P0171 - System Too Lean

 P0171 Toyota-System too lean (bank 1)

        Ni code ambayo ukipima utaipata  kwenye magari ya kampuni ya Toyota  aina karibia zote yanayotumia mafuta aina ya petrol  ikiwamo Ist,Passo,Prado,Rav4 etc,na code hii inamaanisha mfumo wa mafuta/hewa unakuja kwenye injector nozel kwa kiwango kidogo au kuna kiwango kikubwa cha hewa kinakuja ila kuna kiwango kidogo cha mafuta kinasafiri kutoka kwenye pump ya mafuta

                       DALILI ZAKE: 

      Wakati gari ikiwa imewaka au wakati inatembea itakuwa inakosa nguvu na wakati mwingi engine kutetemeka ikiwa imesimama.Kama code hiyo itakuwa inasababishwa na kuvuja kwa hewa unaweza ukawa unasikia mlio wa pssssss  wakati gari limewaka.

Na dalili nyingine ni wakati gari inatembea unaweza kusikia mlio kama wa engine kugonga au wakati inapanda mlima ukikanyaga pedal ya mafuta utasikia gari linabunda


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

P1603 Engine stall history